Introducing Otsieno Godrick, our Translator
The following article on the history of Kenya has been translated by Otsieno Godrick. This issue carries the first article by Godrick. Future issues will carry more. Otsieno translated the first article, Uhuru na Ukoloni Mamboleo: Tusiwai Nyamaza in 2021 for use in his Study Group. Otsieno Godrick, a young activist, symbolises today’s youth in their struggle against capitalism and imperialism. The Editors are grateful to him for translating these articles out of his interest in studying, discussing and disseminating the working class history of Kenya.
Uhuru na Ukoloni Mamboleo: Tusiwai Nyamaza (2006)
Imetafsiriwa na Otsieno Godrick Dondoo. Never Be Silent, Publishing and Imperialism 1884-1963. By Shiraz Durrani. 2006. Nairobi: Vita Books. Chapter 7, pp. 233-238 (selection). Mapambano ya kivita na kisiasa yaliondelezwa na MAU MAU mwishowe yalilazimisha mabadiliko katika sera za kikoloni za Uingereza, si Kenya pekee, bali katika nchi nyingine zilizokoloniwa pia. Kutokana na kuuongezeka kwa visa vya kivita, wakoloni walilazimika kutafuta mbinu mpya za kuendeleza ukoloni. Ingawaje ni kweli vikosi vya MAU MAU vilishindwa kivita, mafanikio yao yalidhihirika. Wakipambana na adui aliyekuwa na rasilimali za himaya, vikosi vya MAU MAU vilifaulu kudhibiti wakoloni kwa Zaidi ya miaka mitano. Wengi hawajafahamu kwamba MAU MAU walishinda vita vya kisiasa vya Uhuru. Kuelekea mwisho wa 1960, ilikuwa dhahiri kwamba uhuru lazima ungepatikana. Hii haingejiri bila miaka mingi ya mapambano na wanavita wa MAU MAU. Lakini vita vya uchumi bado havijashindwa. Wakoloni waliokuwa wakiondoka walijiunga na wabeberu wa Amerika, na hawakuwa tayari kuachilia uendeshaji wa uchumi kwa Kenya ama nchi yoyote iliyokuwa chini ya utawala wa kikoloni zilivyoendelea kupata Uhuru. Mapambano yakawa sasa ya kiuchumi na kisiasa. Hongera inafaa ipewe kwa MAU MAU kwa kutambua hivi na kuanza kupambana na hali hii. Kukielekea mwisho wa miaka ya 1960, sura mpya ya MAU MAU iliendelea na mapambano kwa kuchapisha na kugawa maandishi endelevu ili kuzuia fikra za kikoloni kucheza kwenye uga bila mpinzani. Ili kupinga propaganda za kikoloni na kutilia mkazo umuhimu wa kuendelea na mapambano, wafuasi wa msimamo wa Kimaathi walitayarisha na kuchapisha mawazo, hisia na mtazamo wao kuhusu matukio ya historia, wakitumia maono ya wafanyikazi wa tabaka la chini. Hii ilikwa kwa njia ya nakala zilizosambazwa kwa upana hai kwa mkutano wa KANU uliofanyika Nairobi, Desemba, 1961. Muktadha ulizua aina mbili ya mapambano yaliyokuwa yakitekelezwa ndani ya KANU- ya uhuru wa kweli, ardhi, uhuru wa bender ana dhidi ya ukoloni mambo-leo. Nakala Inaanza na uchambuzi wa mapambano yanayoendelea. Mapambano ya Maisha ya usoni ya Kenya yanaendelezwa leo katika maeneo matatu tofauti lakini ambayo yanaambatana; Kisiasa, Kirangi, na Kiuchumi. Inaonekana kwetu kwamba sisi waafrika tumeruhusiwa kushinda kwa mbili za kwanza, lakini tusishiriki katika mashindano kwa ya tatu, ambayo ni muhimu zaidi, mapambano ya Kiuchumi. Tangu mwisho wa vita vya pili vya Dunia, Waingereza, wakifahamu kuwa hawangedhibiti mawimbi ya mapambano dhidi ya wazalendo wa kitaifa kote kwenye ulimwengu wa kikoloni, waliamua kuelekeza marengo ya kizalendo kwenye njia ambayo ingekuwa nzuri kuendeleza ukoloni wa Waingereza, pamoja na utawala wa mitaji ya kitaifa. Ukoloni wa kitambo uliohusisha utawala wa kisiasa wa kizungu unakufa haraka na mabadiliko ya haraka kuelekea aina mpya ya ukoloni, imeonekana ni lazima ili kuepuka mapinduzi ya kijamii ya kweli, ambayo yatafanikisha uhuru wa kiuchumi, Pamoja na kisiasa na kukomesha mtaji wa ziada wa Kenya kumiminika kwenye benki za wabepari wa kule magharibi. Mpango mkuu wa Waingereza basi ni mwepesi kwa sera: “Kwa umakinifu, peana uongozi wa kisiasa kwa watu waliotekwa kimawazo sawa sawa ‘aina nzuri’ ya mwafrika, yaani wale ambao hisia na masilahi yao ni sawa na yetu, ndio tubaki na udhibiti wa uchumi.’ Kwa kifupi, Waingereza walitaka kuondoka kwa njia kisiasa ili wafadhili wao wa kibepari wabaki wakimiliki uchumi.” Ukieka kama kauli mbiu, mpango huu ungekuwa: “ONDOKA ILI UBAKI.” Basi wacha sisi tupambane na utulivu ambao ni sawa na kurudi kinyumenyume, acha tupambane tukomboe hifadhi kubwa ya ubunifu ambayo sasa imebaki ikilala miongoni mwa watu wetu; acha sisi kwa ufupi, tujenge jamii mpya ambayo inaruhusu kila mtu kuwa na haki ya kula, haki ya kuvuna matunda ya jasho lake, haki ya kuvaa nadhifu, nyumba, na masomo kwa Watoto wao, haki, kwa ufupi, ya kuishi kama binadamu wengine walio tulio sawa nao. Hii ni jamii ya kisoshilisti ambayo tunafaa kupambana kujenga, mfumo ambao kinyume na ubepari, unajihusisha na ustawi wa mwananchi wa kawaida na si faida na upendeleo kwa wachache. Mbinu nyingine inayotumiwa ili wakoloni waondoke wakibaki inaitwa Utaifa. Hii ni itikadi ya kibadala ya ukoloni. Utaifa ni falsafa mbovu na haiwezi kuwa suluisho. Waingereza wamejaribu kutumia hii kauli mbiu mbovu ya kisiasa (wamemaarufisha wenyewe) ili kusimamisha au kuzima kuibuka kwa itikadi ya mapinduzi, ambayo waliogopa ingemaanisha mwisho wa utawala wao wa kikoloni. Yafaa basi tujenge itikadi ambayo italeta umoja kwa watu wengi, kupitia njia ya kuzungumzia mahitaji yao na kuendeleza mpango wa maendeleo ya kisosholisti katika sekta ya kilimo ambayo inaahidi kumaliza umaskini, magonjwa na kutojua kusoma na kuandika, mpango ambao utavuta talanta za ubunifu na nguvu za watu wetu, kuwapa hiyo heshima ya kibinadamu na majivuno ambayo huja kutokana na kujenga jamii na vitendo vya faida kwa jamii. Yafaa, kwa kifupi, tupe watu wetu ala ya itikadi na ushirika ambayo itafanikisha mafanikio ya Uhuru wa kweli na maendeleo. Acha sisi tusiwauze kwa bei mbovu, kwenye njia inayometameta ya ukoloni mamboleo na kusitisha maendeleo ya kijamii, kiuchumi na utamaduni. Huu ndio ulikwa msimamo wa kiitikadi wa MAU MAU pindi kabla ya Uhuru. The selection has been translated from: Never Be Silent